UVIKANJO

UVIKANJO ni Umoja wa Vijana Katoliki Jimbo la Njombe ulioanzishwa mwaka 1971.

Madhumuni na Malengo ya Uvikanjo

 1. Kujenga msingi bora wa imani ya Kikristo katika vijana ambao ni Kanisa la leo na kesho.
 2. kuhakikisha kwamba kila mwanachama anaishi kadiri ya mwongozo wa Yesu Kristo na Kanisa Katoliki.
 3. Kujiendeleza kimwili na kiroho kwa kujifunza mbinu mpya za maendeleo.
 4. Kushiriki kikamilifu wajibu wa kikristo.
 5. Kujenga uhusiano bora kati ya vijana wa parokia yake na parokia nyingine na wa jimbo zima na wa madhehebu mengine.
 6. Kujenga uhusiano bora kati ya vijana wa vyama vya siasa na serikali na vyama vya vijana.

KATIBA YA UVIKANJO INASEMA NINI?

Vijana wenyewe tukitambua umuhimu wa utume wetu tunasema:

“Sisi vijana wakatoliki Jimbo la Njombe tunatambua kwamba:

 • Tuna wajibu mkubwa kwa Kanisa na Taifa.
 • Nguvu na vipaji vyetu vihudumie Kanisa na Taifa.
 • Tukiongozwa na imani ya Kikristo na Viongozi wetu pamoja na wazee wetu, sisi wenyewe ni mitume miongoni mwetu. (Taz. Vat.II, Walei 2,12)

SHUGHULI ZA VIJANA

I. Kiroho

 • Kuongoza liturujia kwa kuimba na kusoma masomo kanisani.
 • kusoma maandiko matakatifu
 • kuwatembelea wagonjwa na kuwafariji wenye shida mbalimbali.
 • kufanya uchungaji kuhamashana wenyewe kwa kutembeleana vigangoni na parokiani.
 • kuwashauri wanaokaa uchumba ili wafunge ndoa.
 • kuwasaidia wazee na wenye shida mbalimbali.
 • kushiriki semina mbalimbali.
 • kufanya hija na makongamano.
 • kusimamia shughuli za Utoto Mtakatifu jimboni.

II. Kimwili

 • Upandaji wa miti.
 • Ujenzi wa Kanisa la Kiaskofu Jimboni.
 • Kusaidia ujenzi wa kituo cha vijana cha Nazareti.
 • Kusaidia ujenzi wa Seminari ya Kilocha.
 • Kulima mashamba ya vikundi kama chai.
 • Vikundi mbalimbali vya ushonaji, ufugaji, useremala, uvuvi na ufinyanzi.
 • Vyuo vya ufundi na karakana.