Idara na Vitengo

Idara


Uchungaji

Uchungaji

"Nendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi wangu" (Mt. 28:19)
Idara hii hushughulikia mambo mbalimbali ya kichungaji katika Jimbo Katoliki la Njombe kwa ajili ya wokovu wa roho za watu kadiri ya agizo la Bwana wetu Yesu Kristo yakiwemo Halmashauri ya Walei na vyama vya Kitume. Vyama vya Kitume vilivyopo jimboni kwa sasa ni: UVIKANJO, TYCS, WAWATA, Moyo Mtakatifu wa Yesu, Legio Mariae, Utume wa Fatima, ME, CPT, Utoto Mtakatifu, UWAKA.
Mkurugenzi wa Idara hii ni Pd. Francesco Betesi CHENGULA

Soma Zaidi

Miito Mitakatifu

Miito Mitakatifu

Hazina kubwa ya Kanisa ipo katika Miito Mitakatifu ya Upadre na Utawa. Katika Jimbo la Njombe kuna mapadre wazalendo 109 na pia kuna watawa mashirika mbalimbali yenye karama anuwai ziletazo utajiri wa wanafamilia ya Mungu.
Mkurugenzi wa Miito: Fr. Lucas Mgaya

Soma Zaidi

Liturujia

Liturujia

Kanisa Katoliki linafanya daima kazi ya kuwaunganisha waamini wake na Mungu kwa njia ya maadhimisho na ibada mbalimbali kupitia makuhani wake walioteuliwa kutoka kwa watu kwa ajili ya watu katika mambo yamhusuyo Mungu.
Mkurugenzi: Fr. Crispin Yalila MWAGENI

Soma Zaidi

NDO Logo

Caritas & NDO

Utume wa Kanisa Katoliki huhusisha pia kuwaelimisha na kuwasaidia watu katika maisha yao ya kila siku ndani ya jamii wanamoishi. Hivi kwa kupitia Idara ya Caritas na NDO Kanisa linatoa mchango mkubwa wa kuwainua waamini kiuchumi kwa kuwajengea na kuwapa miradi ya maendeleo.
Mkurugenzi: Fr. Hermengird LUGOME

Treasurer

Ofisi ya Mhasibu

Mhasibu wa Jimbo: Fr. Camillo MDEYA
Wasaidizi: Fr. Arnold NGOLLE na Fr. Fortunatus MWINUKA
Waweka hazina: Sr. Edmara MKALAWA OSB na Sr. Prisca OSB

Annunciation

Habari na Mawasiliano

Idara hii inafanya kazi ya kuratibu habari na Mawasiliano jimboni na nje ya Jimbo la Njombe.
Mkurugenzi: Fr. Bruno HENJEWELE

Health

Afya

Kwa kuwa binadamu ni mwili na roho, Kanisa linazingatia sana mambo yote mawili. Idara hii inaendesha shughuli zake ili kuokoa na kuponya mwili wa mwanadamu kwa njia ya huduma za hospitali, vituo vya afya na zahanati zilizojengwa na zinaendeshwa na jimbo.
Mkurugenzi: Fr. Fortunatus MWINUKA
Katibu: Ms Christina CHONGOLO

kongamano

Elimu

SERA YA ELIMU JIMBONI NJOMBE: "Elimu na Malezi bora"
Elimu na malezi bora ni msingi maisha ya mwanadamu yeyote ili aweze kuendelea kimwili na kiroho. Idara ya Elimu Jimbo inaweka msisitizo katika elimu iliyosheheni malezi bora. Kwa kuzingatia hili Jimbo limeanzisha shule za chekechea, msingi, sekondari na vyuo mbalimbali ili kukidhi sera yake ya elimu.

Miradi


Water

Maji

Umeme

Umeme

Msimamizi: Fr. Fortunatus MWINUKA

Mawolo

Chai

Meneja: Fr. Arnold NGOLLE