MOYO MTAKATIFU WA YESU

Shirika la Moyo Mtakatifu

Neno Moyo lina matumizi mengi. Mara nyingi tumesikia watu wakisema dada yule ana moyo mzuri ..nakupenda kwa moyo wangu wote,matendo yake yamenitia moyo nk.Watu hutumia Moyo wakiwa na maana ya kuonyesha Nia, makusudio na zaidi sana kile kinachomsukuma mtu kufanya jambo Fulani.TUJIULIZE NINI KILIMSUKUMA Yesu kuja duniani kuteswa kudharauliwa na kufa kifo cha aibu msalabani?…….. Hakika si kingine bali ni UPENDO WA MOYO WAKE MTAKATIFU. Moyo wake kwa asili ni Moyo wa upendo na matunda ya upendo wa moyo wake ni huruma unyenyekevu upole msamaha wa dhambi .

Maneno ya Yesu, “Makusudi ya moyo wangu ni kwa kizazi na kizazi” “Kama vile baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, Kaeni katika PENDO langu” (Yn 15:9). “Kaeni katika MOYO wangu”

Kutoka katika Moyo Mtakatifu wa Yesu mtateka maji ya Wokovu, maji ya Uzima. Mtateka Sakramenti za Pasaka, Sakramenti za Uzima na Neema. Huruma na Rehema, Msamaha na Upendo. Moyo wa Kristo ni kina cha Upendo wa Mungu kwa ajili ya kugusa kina cha Moyo wa Binadamu na kuujaza Upendo wa milele wa Mungu na Uzima wa milele wa Mungu.

A. MAUDHUMUNI YAKE

 • Kumrudishia mapendo Moyo Mtakatifu wa Yesu aliyetupenda sana
 • Kufanya Malipizi ya dhambi zetu na za dunia nzima
 • Kusimika ufalme wa Kristo katika nyoyo za wanachama, na katika nyoyo za ndugu zao wa nchi hii, na katika dunia yenyewe. Kwa kifupi ni kufanya bidii yoyote ile wanayoweza kufanya ili watu na vitu vyote vimwungame Yesu kuwa Mfalme wao.

WAJIBU

 • Kujitolea kila siku unapoamka asubuhi kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu katika sala na kazi. Na kubwa ni kuepa dhambi Sala fupi ya kujitolea kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu.
  Ee Moyo Mtakatifu wa Yesu, Mimi (…)Najitolea leo na siku zote za maisha yangu kwako. Mimi ni mali yako, na kila nilicho nacho nakitoa kiwe mali yako.
 • Kupokea Sakramenti ya Kitubio mara kwa mara.
 • Kushiriki Misa na kupokea Ekaristi Takatifu mara nyingi iwezekanavyo na hasa siku ya Ijumaa ya kwanza ya mwezi.
 • Kuhudhuria saa Takatifu yaani kuabudu Alhamisi/Alhamisi inayotangulia Ijumaaya kwanza ya mwezi.
 • Kuhudhuria na kupokea Ekaristi Takatifu Ijumaa ya kwanza ya mwezi na hasa ijumaa 9mfululizo ili kufaidika na ahadi 12 alizoweka Bwana wetu Yesu Kristu
 • Kufanya malipizi kwa ajili ya dhambi na makosa yako na ya watu wa jamaa zako na ya ulimwengu mzima.
 • Kuwa na nia ya kutotaka kuuchikiza Moyo Mtakatifu wa Yesu kwa dhambi yoyote. Kutokawia katika dhambi na kufanya maelekeo ya ukamilifu.
 • Kuwaenezea ndugu wengine ibada ya ufalme wa Moyo Mtakatifu wa Yesu na kwa ndugu wengine wasio bado na ibada hiyo.

C. UANACHAMA

Mristu yeyote asiye na kizuizi.yaani anayeshiriki masakramenti. Kwa maneno mengine;-

 • Kama ni mtu wa ndoa anapaswa kuwa na amani na mapatano na mwenzi wake.
 • Wazazi wanapaswa pia kuwa na amani na watoto wao, aidha wawe mfano bora kwa jamii.
 • Mvulana au msichana awe na mwenendo mwema na sifa nzuri kati ya watu.