JUBILEI YA MAPADRE JIMBO

Tarehe 11 Oktoba 2018 ni siku rasmi kwa Jimbo la Njombe kuadhimisha na kusherekea Jubilei za mapadre wake wa Jimbo. Jubilei hizo zaweza kuwa miaka 25,50,75 au 100.
Mwaka huu Jimbo la Njombe lilibahatika kupata mapadre wanne (4) waliotimiza miaka 25 ya utume wao kama mapadre ndani ya Jimbo. Mapadre hao ni hawa wafuatao:
1. Pd. Alois Msigwa toka Parokia ya Matembwe
2. Pd. Arnold Ngolle toka Parokia ya Utalingolo
3. Pd. Bernwald Mlowe toka Parokia ya Lugenge na
4. Pd. Clement Mgohele toka Parokia ya Kipengere

Misa hii iliongozwa na Mhashamu Askofu Alfred Maluma, Askofu wa Jimbo Katoliki la Njombe. Katika mahubiri yake Baba Askofu aliwaasa mapadre wajubilanti kujitafiti nafsi zao na utumishi wao wa miaka 25 kama mapadre wa Kanisa Katoliki. Pia ni nafasi ya kuhuisha viapo vya upadre. Katika kuhuisha viapo vya upadre mapadre wafanye tathmini ya kazi yao ya miaka yote hii kwa kuweka balance sheet ya mambo ambayo wamefanya kwa kipindi hiki. Kama mapungufu yanazidi zaidi ya mambo mazuri basi utumishi wao unashida kubwa.Ikiwa mazuri yanazidi mapungufu basi utumishi wao upo vizuri.

HITIMISHO LA MWAKA WA JUBILEI YA MIAKA 15O YA UKRISTO TANZANIA BARA
Siku hiyohiyo Jimbo la Njombe lilifanya hitimisho la Jubilei ya miaka 150 ya Ukristo Tanzania Bara. Baba Askofu alisisitiza kwamba Kanisa ni sisi wenyewe na litategemezwa na sisi wenyewe. Akawaalika waamini kujitoa kwa moyo ili kulitegemeza Kanisa.

UZINDUZI WA JUBILEI YA MAPADRE WANAOFUATA
Katika tukio hili pia kulifanyika uzinduzi wa Jubilei ya Miaka 25 ya Mapadre wanaofuata kwa urika kwa ajili ya mwaka 2019. Mapadre hao walipewa mishumaa ya Jubilei inayowaka (nuru itakayowaangaza wawapo katika hija yao mwaka mzima), na mwisho walipewa baraka ya mwanzo wa mwaka wa Jubilei na Mhashamu Askofu Alfred Maluma.
Mapadre hao ni:
1. Fr. Ado Mwageni
2. Fr. Claudius Nkwera
3. Fr. Gaufried Mwanyika
4. Fr. Johnbosco Mwinuka
5. Fr. Marianus Nziku
6. Fr. Renatus Mwalongo
Tuwaombee katika hija yao ya mwaka wa Jubilei.