JIMBO LA NJOMBE LAPATA SHEMASI NA MAPADRE


Tarehe 11 Januari 2018 ilikuwa na siku ya furaha kwa Jimbo Katoliki la Njombe ambapo Mhashamu Askofu Alfred Maluma alitoa Daraja Takatifu ya Ushemasi kwa Mseminari Oswald Mgaya wa Parokia ya Kipengere na Daraja ya Upadre kwa Mashemasi Frank Mwinami wa Mtwango na Johnbosco Mligo wa Parokia ya Njombe.
Katika mahubiri yake, Askofu Maluma aliwasisitizia wateule kuingia katika Daraja Takatifu kwa udhati wa dhamiri na mioyo yao na kwa umakini (with due seriousness). Wajitahidi kuishi vema upadre wao ili wasiwe ni mzigo kwa Kanisa. Wawe ni mtaji wa Kanisa.

Watumie muda na mali zao kwa ajili ya Mungu na Kanisa. Mungu awe na nafasi ya kwanza katika maisha ya kila siku ya Mkleri. Hali Kadhalika Kanisa na waamini wapewe kipaumbele katika maisha ya mkleri.

Mwishoni Mhashamu Askofu Maluma aliwaomba waamini kuwaombea mapadre katika utume wao wa kila siku.