Makongamano ya UVIKANJO Kidekania yasisimua vijana

Hivi karibuni kumekuwepo na makongamano ya Vijana wanaUVIKANJO katika dekania mbalimbali za Jimbo la Njombe. Dhamira iliyokuwa inaongoza makongamano hayo ni: MKUMBUKE MUUMBA WAKO SIKU ZA UJANA WAKO (Mhubiri 12:1). Vijana wengi wamejitokeza kuhudhuria makongamano hayo ambayo yaliandaliwa na dekania hizo kwa ushirikiano na Ofisi ya Vijana Jimbo. Makongamano haya yamekuwa ni chachu ya kuwaleta vijana pamoja na kufanya mambo yao kwa pamoja. Vijana wamekuwa wakipata mada zifuatazo:
1. Nafasi ya Kijana katika Kanisa na Jamii.
2. Makuzi ya Kijana katika ulimwengu wa sasa.
3. Ujasiriamali
Vilevile, vijana walikuwa wakishindana katika mambo mbalimbali kama vile:
1. Maandiko Matakatifu
2. Wimbo wa Dhamira (Mkumbuke Muumba wako Siku za Ujana wako)
3. Mpira wa Miguu
4. Mpira wa Pete
5. Riadha
6. Kuruka kamba na viunzi
7. Ngoma za utamaduni
8. Muziki wa Kizazi kipya
9. Maigizo mbalimbali yenye dhana ya Kibiblia.
Naye Mhashamu Baba Askofu Maluma alikuwa daima akipita kuwasalimu na kuimarisha vijana katika utume wao. Aliwahakikishia vijana kuwa Kanisa linawajali, linawapenda, linawathamini na linawategemea. Daima wawe ni nguzo na mtaji kwa Kanisa lao. Wasiyumbishwe na upepo na mafundisho yasiyo na msingi ya madhehebu mengine yasiyo na mwanzo wala hakuna utaratibu.